VISA
NA MAFUNZO,
Nilipoanza safari ya
kukuandikia wewe msomaji,nilivuta picha ya jambo ninaloenda kulileta kwako.Ama
kweli kuna vitu visivyozuilika,na uchungu
pia, upo katika “list” ya vitu visivyozuilika. “hivi kwanini nadondosha
chozi?” nilijisemea na kujiuliza kwa muda,hatimaye “ ngoja nijikaze tu!”
nilijipa imani nikiamini kuwa huu sio mwisho wasafari,huenda nami
yakanikuta “kama nilisimuliwa pia
nimejionea kwa macho yangu,imetokea kuumia namna hii,je,si zaidi kama
ikinitokea mimi la!”nilijisemea na kujiuliza pia.Gafla nilizikumbuka jumbe
ambazo zimetikisa katika kichwa,nazo pia zipo ndani ya malengo niliyo nayo juu
yako msomaji,nilianza kujipa tumaini kwa mbali nikiamini utaenda kukumbana na
yaliyomengi ndani ya kijitabu hiki. “Hivi kwa nini
ulimfanyia hivyo? Kipndi chote hicho
haukutambua kuwa maisha yake umeyashikilia
mikononi mwako? Umeridhika kuona anataabika na amepoteza mwelekeo na dira kabisa ya maisha yake!” Kuna tofauti kubwa kwa mtu Yule anayeliona tukio na
kushindwa kulipa nafasi ya kulitafakari
kwa kina,na mtu Yule anayeliona tukio na kulitafakari kwa kina.Kabla
sijakupeleka katika ukurasa mwingine wa
maandishi,naomba nikupe kisa kimoja ambacho sio yeye tu,ni wengi
huwapata.Alikuwapo mtu mmoja ambaye
alitembelewa na rafiki yake Asubuhi na
mapema.Kama ilivyokawaida,alimkaribisha
rafiki yake kwa furaha na shangwe ya hali ya juu.Walishinda nyumbani
pamoja huku wakiendelea “kucheas” pamoja.Mara huyo mchana, na hatimaye jioni
“karibu tena” mara alimwaga na kumkaribisha
kwa mara nyingine .Akiwa njiani alikutana na jamaa
mwingine,walisalimiana na hatimaye waliagana.Kwa kuwa jamaa huyo alikuwa mtani
wa rafiki yake aliyetoka kumtembelea
aliona ni njia pekee ya kumtania kwa kiswali ili akishindwa aweze
kumzomea.Haraka alifika kwa mtani wake
“hongera chalii
wangu,leo umekuwa ma mgeni
(alijibu)
Mara aliulizwa kiswali cha utani,
“hivi mgeni
wako alikuwa amevaa nguo ya rangi gani?
Je,vipi kuhusu viatu vyake?” ndugu msomaji unaweza kuona swali hilo ni la
kipumbafu muno,japokuwa lina maana yake.Mtani alijitwalia ushindi.Swali hilo
lilileta utata na hatimaye kuzomewa.Huo ndio uhalisia wa maisha kutokana na
vitu au mambo tunayo kutana nayo na kuyaona.Pengine angejipa muda wakufikiria
mgeni aliyefika pale nyumbani na
kushinda naye kutwa nzima,sina shaka ,swali hilo lingekuwa rahisi muno.Simlaumu
kwani hakujipa muda wa kufikiria kwa undani,ujio wa rafiki yake pale
nyumbani.Laiti kama angewaza,angefikiri,angechunguza kwa kina,angegundua
masuala mengi juu ya rafiki yake.Suala la kushindwa kutambua rangi ya nguo au
viatu,lisingeweza kumpata chalii huyo.
Nikukaribishe katika ukurasa mwingine
wa maandishi,kisa hicho hakiko mbali na jambo ninalolileta kwako,ni jambo
rahisi na la kawaida sana.Japokuwa linahitaji kufikiria na kutafakari kwa
undani zaidi.Suala la kuliona halina mguso au lina mguso liko juu yako wewe
msomaji.
TAFAKARI
yako itakupa radha ya utunzi wa kijitabu hiki “Bado
naendelea kukuuliza hivi kwa nini ulimfanyia hivyo? Kipindi chote hicho
haukutambua kuwa maisha yake umeyashikilia mikononi mwako? Umeridhika kuona
anataabika na amepoteza mwelekeo na dira kabisa ya maisha yake!!”
Ukurasa huu wa maandishi umeambatana na ushauri kwako
wewe msomaji.Pengine unapenda kujifunza kitu kupitia maandishi haya.Pengine
unatamani kuwa jasiri pale unapotaka
kuanza safari ya maisha yako.Pengine unakatishwa tamaa na hatimaye kupelekea
kufa na maono yaliyoko katika kichwa chako,sina shaka kuwa ukinisikiliza mimi
,hutoweza kuanguka kwani sina rekodi ya watu walionisikiliza na kujulikana kuwa wamepotea kwa kufuata ushauri wangu.Ndugu
tumia “KITABU
WATU” hiki ni kitabu
ambacho kimeutoa msaada mkubwa ndani ya safari yangu .Ni kitabu ambacho kimetoa
faraja kubwa na tumaini katika maisha yangu.Ni kitabu pekee kinachopatikana
kila kona ya dunia,kila unapokaa,kitabu hiki utakipata,kila unapotembea,kitabu
hiki kipo palepale.Halooo! kila kona,kitabu hiki hujifunua zaidi kukufundisha
wewe msomaji wangu.Tumia “ KITABU WATU” kitabadilisha msimamo wa maisha yako.Natumia
muda mwingi kuwasoma watu ambao wamepiga hatua Fulani kimaisha,wengine ambao
wamenitangulia kutimiza ndoto kama
nilizonazo “Ahsanteh sana Erick Shigongo,street university,umekuwa kitabu bora
na umebadilisha mitazamo ya maisha yangu.Maisha yako nimeyageuza kuwa ukurasa
wa kitabu,kila siku najitahidi kufungua ukurasa mmojammoja,na kuendelea
kujifunza mengi na mengi.Tumia “KITABU
WATU” kitabadilisha
msimamo wa maisha yako.Unaamini kuwa palipo na vitoto vichanga,katikati yao
kuna kiongozi,unaamini wanyama wa mbugani katikati yao kuna kiongozi,unaamini
katika msululu wa siafu pia kuna kiongozi? Kama ndiyo,utaniambia hapo ulipo
hakuna mtu yeyote wa kugeuza kuwa ukurasa wa kitabu,kila siku ukaufunua na
kuendelea kuongeza maarifa? Tumia “KITABU WATU” kitabadilisha msimamo wa maisha
yako. “Bado
naendelea kukuuliza kwa nini ulimfanyia hivyo? Kipindi chote hicho haukutambua
kuwa maisha yake umeyashikilia mikononi mwako?umeridhika kuona anataabika na
amepoteza mweleleo na dira kabisa ya
maisha yake!”
“Unyoya
haumdondoki ndege pasina sababu,utamu wa kitabu si maandishi la! Kilichomo ndaniyake,tafakari
ni zaidi ya takabari.Hana maana mkosa vyote ajisifupo “nalikuwa nao wapataji tulipo
tafuta pamoja”.Thabiti ya neno ni shahada si shuhuda pia salama ni tathimini ya
imeishaje” ukweli wa semi hizi mpenzi msomaji bila
kukuchosha,utaupata baada ya kusoma visa vyote ambavyo utakumbana navyo ndani ya kijitabu hiki.Pengine bado una shauku ya kutaka kujua ,taratibu tutafika
sehemu ile ya kupata ukweli wa semi hizi. “Bado naendelea
kukuuliza kwa nini ulimfanyia hivyo?kipindi chote hicho haukutambua kuwa maisha
yake umeyashikilia mikononi mwako? Umeridhika kuona anataabika na amepoteza dira
na mwelekeo kabisa wa maisha yake!”
Mpenzi
msomaji,nisikuchoshe,tulipate funzo kidogo,baadae nikupeleke katika vile visa
ambavyo vimenisukuma kuandika kijitabu hiki.Jana nilifunga safari na kwenda
kumtembelea mzee wangu,sio mzee sana ,hajawa mzee wa makamo,nusu mzee nusu
kijana japokuwa anaelekea uzeeni.Ni tegemezi si tegemezi maana yake uchumi wake
ni wa kati.Nilikaa nae muda mrefu,baadaye alianza kunipa mawaidha alisema
“mchana huu ningekuwa mbali sana,sijui ningekuwa wapi,kama si katika michakaliko
basi ningekuwa kwenye starehe ila kama unavyoona,nipo nyumbani nimekaa.Sina
nguvu tena,ujana ni muda tu.Ningepata nafasi ya kuambiwa kilichoko
uzeeni,haloo,ningepambana kupata ili nije nitumie uzeeni,nisingepika
mbegu,ningepanda mbegu na kuimwagilia
ili nije nivune uzeeni lakini muda umepita,natamani kuwa kama wewe kijana
japokuwa haiwezikani.Kijana tumia ujana wako vizuri maana umejionea kilichoko
uzeeni,alimalizia kwa kusema
“mkumbuke
muumba wako siku za ujana wako,
Kabla hazijaja siku zilizo
mbaya,
Wala
haijakaribia miaka utakaposema,
Mimi
sina furaha katika hiyo,
Kabla
jua na nuru na mwezi,
Na
nyota,havijatiwa giza,
Kabla
ya kurudi mawingu baada ya mvua,
Siku
ile WALINZI WA NYUMBA watakapo tetema,
Hapo
wenye nguvu watakapojiinamisha ,
Na
wasagao kukoma kwa kuwa ni haba,
Na
hao wachunguliao madirishani kutiwa giza,
Na
milango kufungwa katika njia kuu,
Sauti
ya kinu itakapokuwa ni ndogo,
Na
hao binti za kuimba watakapopunguzwa” Mzee wangu hakunikaribisha na vinywaji
,vyakula kama wengine wafanyavyo ila tunda alilolipandikiza katika kichwa
changu,lilinifanya nipendezwe na ugeni wangu.Jana hiyohiyo sikwenda ukumbi wa
starehe nilishinda nyumbani sebuleni nikiwaza yaliyomengi. “Bado
naendelea kukuuliza hivi kwa nini ulimfanyia hivyo? Kipindi
chote hicho haukutambua kuwa maisha yake umeyashikilia mikononi mwako?
Umeridhika kuuna anataabika na amepoteza mwelekeo na dira kabisa ya maisha
yake!!”
Nilimsikia
mwingine akisema “sitaki nipate ‘certificate’ ambayo itanipa mzigo maishani mwangu”
baada ya kusikia hivyo nilijiuliza ni nini maana ya kile akisemacho,
“certificate ni kitu kizito mpaka kiwe mzigo namna hiyo?” sikukawia,nilimfuata na kumuuliza “vipi uzito wa ‘certificate uko wapi ndugu
yangu maana nimesikia ukisema hutaki upate ‘certificate’ ambayo itakupa mzigo
maishani mwako.’’ Alinicheka sana ,nami pia nilijiona mtu wa ajabu muno. Kwa
kuwa nia yangu ilikuwa ni kutaka kujua,sikukata tamaa nilimuomba anieleze ni
nini alimaanisha.Aliniambia “sitaki nipate kazi ambayo haitaleta furaha
maishani mwangu,haijalishi kazi hiyo ni ndogo au kubwa.Natamani nipate kazi
ambayo italeta furaha maishani mwangu,naamini nitaridhika nayo hata kama mapato
yake yatakuwa ni madogo.Nafanya uchaguzi wa kazi ya kufanya kwanza ili nisije
nikanung’unika kwa maisha ya baadae” Ahsanteh sana ndugu yangu nimekuelewa
wanena vyema,sikujua ndugu yangu nimelipata funzo ahsanteh sana. “Bado
naendelea kukuuliza hivi kwa nini ulimfanyia hivyo? Kipindi chote hicho
haukutambua kuwa maisha yake umeyashikilia mikoni mwako?umeridhika kuona
anataabika na amepoteza mwelekeo na dira kabisa ya maisha yake!”
Msomaji,siku
moja nilikaa na kuwaza hivi kwa nini baadhi ya watu hujikana wenyewe na kuamua
kufanya vitu au mambo ambayo hayana mchango wowote kwa maisha ya baadae.Wengine
hupelekea kukata tamaa na kuamua kila wapatapo vijisenti huishia ‘lodge’,pombe
ubadilika kuwa kinywaji cha kutulizia kiu,namaanisha ulevi wa kupindukia,maisha
yao huwa hayana tumaini tena katika mioyo yao.Nilipoanza kufatilia na kufanya
uchunguzi nilitambua ya kuwa kweli “unyoya
haumdondoki ndege pasina sababu”.Visa ambavyo napenda nikuletee
vimeambatana na swali ambalo naamini mpaka kufikia ukurasa huu wa kijitabu hiki
umekumbana nalo mara kwa mara “Bado
naendelea kukuliza hivi kwa nini ulimfanyia hivyo? Kipindi chote hicho
haukutambua kuwa maisha yake umeyashikilia mikononi mwako?umeridhika kuona
anataabika na amepoteza mwelekeo na dira kabisa ya maisha yake!!” sipendi
nikuchoshe sana kwa maandishi mengi pindi nikuleteapo visa hivi kwani naamini “utamu wa kitabu si maandishi la! Kilichomo ndani yake” twende sambamba ,tiririka nami mwanzo mpaka
mwisho,usiachwe hata nukta pindi usomapo visa hivi.
Mlio wa filimbi ukilia,lazima
ujiulize kunani?.sauti ya Bigola ikisikika,jemedari huwasiri haraka sehemu
husika.Basi nami huu ndio muda wa kukufungulia visa ambavyo vimetikisa katika
kichwa changu.Kwa kuwa “tafakari ni zaidi
ya takabari”,nikualike katika ukurasa wa visa hivi ,tuwe pamoja ,tutafakari
pamoja kwani radha ya utunzi huu wa kijitabu hiki iko mikononi mwako msomaji.
“KWA NINI ULIMFANYIA HINYO?KIPINDI CHOTE HICHO
HAUKUTAMBUA KUWA MAISHA YAKE UMEYASHIKILIA MIKONONI MWAKO?UMERIDHIKA KUONA
ANATAABIKA NA AMEPOTEZA MWELEKEO NA DIRA KABISA YA MAISHA YAKE!!”
Kisa cha kwanza;FATILIA MWENDELEZO
Maoni
Chapisha Maoni